Tunajaribu Kugundua Nini?
Moja ya matumizi muhimu ya upimaji wa lactate ni kutambua maeneo ambayo mwitikio wa mwili hubadilika kadri nguvu ya mazoezi inavyoongezeka.
Kwa ufupi, tunataka kuelewa:
Mazoezi ya aerobic — ambapo lactate hubaki katika kiwango cha chini na tulivu
Mazoezi ya threshold — ambapo mwili unafanya kazi kwa bidii lakini kiwango bado kinaweza kudhibitiwa
Mazoezi ya nguvu kubwa ambapo lactate huanza kuongezeka kwa kasi na uchovu huongezeka
Kipimo cha lactate kilichopangwa vizuri kinaweza pia kusaidia kuainisha training zones za mtu binafsi,na kukupa uelewa mzuri zaidi wa kiwango cha nguvu kinachofaa kwa aina mbalimbali za mazoezi.
ambo muhimu ni kwamba maeneo haya ni ya mtu binafsi.Hayapaswi kutegemea tu asilimia fulani ya kiwango cha juu cha mapigo ya moyo kwa kila mkimbiaji.
Ukiwa na Kipima Lactate
Ukiwa na kipima lactate, unaweza kufanya kipimo maalum kwa kuongeza kasi ya kukimbia hatua kwa hatua na kuchukua sampuli ndogo ya damu katika kila hatua.
Kisha unaweza kuangalia jinsi lactate, mapigo ya moyo, kasi na kiwango cha juhudi unachohisi vinavyobadilika kadri nguvu ya mazoezi inavyoongezeka.
Hii inaweza kusaidia kuainisha training zones za mtu binafsi na kutambua viwango vinavyofaa vya mazoezi kwa mkimbiaji.
Kurudia kipimo baadaye kunaweza pia kuonyesha kama mwitikio wa mwili umebadilika — kwa mfano, kama sasa unaweza kukimbia kwa kasi zaidi ukiwa na kiwango cha lactate kinachofanana.
Bila Kipima Lactate
Bado unaweza kutumia kanuni nyingi hizi bila kupima lactate.
Mapigo ya moyo, kasi na kiwango cha juhudi unachohisi vinaweza kutoa taarifa muhimu.
Hata hivyo, ikiwa utatumia mapigo ya moyo kuongoza mazoezi, amna unavyopima mapigo ya moyo ni muhimu..
Kwa mazoezi yaliyopangwa, mimi sipendekezi kutegemea heart-rate inayopimwa na saa kwenye kifundo cha mkono.Kipimo hiki kinaweza kuathiriwa na mwendo wa mkono, cadence, jinsi saa ilivyokaa kwenye mkono na mambo mengine, hasa wakati kiwango cha nguvu kinabadilika haraka.
A Chest strap au heart-rate armband yenye ubora mzuri ni chaguo bora zaidi kwa mazoezi yanayoongozwa na heart rate.
Hii hukupa taarifa ya kuaminika zaidi unapoweka na kufuatilia viwango vyako vya mazoezi.
Jambo Muhimu: Uthabiti
hamani ya upimaji wa lactate si namba unayopata kutoka kwenye kipima pekee.
Ni kuhusu kuelewa mwitikio wa mwili wako binafsi kwa mazoezi..
Iwe unatumia kipima lactate au unatumia mapigo ya moyo, kasi na kiwango cha juhudi unachohisi,lengo ni lilelile:
Fanya mazoezi kwa kiwango sahihi kulingana na lengo la session.
Huhitaji vifaa vya gharama kubwa ili kuwa mkimbiaji bora.
Unahitaji kuelewa kwa nini unafanya session hiyo na unajaribu kufikia nini..
Katika Runners Ascend
katika Runners Ascend,ninaamini data ni chombo cha kutusaidia kuelewa mazoezi — si kitu kinachopaswa kutawala kila kitu.
Upimaji wa lactate ni sehemu moja tu ya picha nzima.
Lactate. Kasi. Mapigo ya moyo. Kiwango cha juhudi. Historia ya mazoezi. Matokeo ya mashindano.
Vitu hivi kwa pamoja vinaweza kutupa picha iliyo wazi zaidi ya mkimbiaji na kusaidia kuainisha training zones ambazo zinaendana zaidi na mtu binafsi.
Pima pale inaposaidia. Sikiliza mwili wako kila wakati. Fanya mazoezi kwa lengo.
